KAULIMBIU:  Kiswahili - Mhimili wa Umoja, Maendeleo ya Elimu na Uchumi.


Zifuatazo ni idara za taaluma za BAKITA na majukumu ya kila Idara; Sehemu ya pili ya Muundo wa Baraza inatokana na Sekretarieti ya Baraza la Kiswahili la Taifa yenye Wakuu wa Idara za Taaluma inayohusika na utendaji wa siku hadi siku wa kazi za Baraza.

BAKITA lina idara 7 ambazo ni hizi zifuatazo:-

 1. Idara ya Uhariri na Uchapishaji
 2. Idara ya Lugha na Fasihi
 3. Idara ya Tafsiri na Ukalimani
 4. Idara ya Istilahi na Kamusi
 5. Idara ya Mawasiliano na Umma
 6. Idara ya Fedha
 7. Idara ya Utumishi na Utawala

Shughuli na Majukumu ya kila idara yameorodheshwa hapo Chini kama ifuatavyo:-


 1. Kutoa huduma za ushauri na utaalamu kwa waandishi chipukizi na wabobezi.
 2. Kuhariri miswada ya kitaaluma na ya kawaida.
 3. Kuchapisha taarifa za kazi za BAKITA, majarida na machapisho mengine ya BAKITA.
 4. Kutangaza, kutafuta masoko na kuuza machapisho ya BAKITA kwa kushiriki katika maonyesho mbalimbali.
 5. Kuratibu mashindano ya uandishi wa insha kwa walengwa anuwai.
 6. Kushiriki katika shughuli za tasnia ya vitabu.
 1. Kusimamia matumizi sahihi ya Kiswahili Sanifu katika vyombo vya habari na matumizi rasmi.
 2. Kutoa ithibati ya matumizi sahihi ya Kiswahili Sanifu kwa miswada ya vitabu vya Kiswahili vinavyokusudiwa kutumika katika elimu.
 3. Kuratibu matumizi na maendeleo ya Kiswahili mikoani, mahali pa kazi na vikundi mbalimbali vya wapenzi wa Kiswahili.
 4. Kufuatilia maendeleo na matumizi ya Kiswahili kwa wageni ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
 1. Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani kwa lugha mbalimbali kwa Mashirika, Idara, Wizara, Balozi na Watu Binafsi.
 2. Kuratibu na kutoa huduma za Ukalimani kwenye mikutano ya Kitaifa na Kimataifa na katika shughuli za mashirika, makampuni na watu binafsi.
 3. Kupitia na Kuthibitisha tafsiri zilizofanywa na asasi mbalimbali au wafasiri wa nje.
 4. Kutoa ushauri kuhusu masuala ya Tafsiri na Ukalimani.
 1. Kufanya utafiti wa istilahi zinazotakiwa kusanifiwa na Kamati ya Kusanifu Lugha.
 2. Kuandaa orodha ya istilahi zinazosanifiwa na Kamati ya Kusanifu Lugha na kuthibitishwa na Baraza.
 3. Kuandaa istilahi sanifu kwa ajili ya kuchapishwa katika matoleo ya Tafsiri Sanifu na kufuatilia matumizi yake.
 4. Kuandaa Kamusi kwa matumizi ya asasi, shule na watu wa aina mbalimbali.
 5. Kutoa ufafanuzi wa istilahi kwa wanaohitaji.
 1. Kusimamia vipindi vya Kiswahili katika redio na televisheni.
 2. Kuthibitisha mahitaji na matatizo ya jamii.
 3. Kupima matokeo ya kazi inayofanyika.
 4. Kupokea maswali, maombi na maoni ya wasikilizaji.
 5. Kutangaza kazi na shughuli za Baraza kwa kutumia redio, televisheni, Magazeti, Majarida na Magazini.
 6. Kusimamia kipindi cha Lugha ya Taifa katika redio.
 7. Kuwa kiungo baina ya Idara na Vitengo ndani ya Baraza.
 8. Kuwa kiungo kati ya Baraza na jamii.
 9. Kuratibu na kuhifadhi kumbukumbu za matukio muhimu ya Taasisi.
 10. Kuisemea Taasisi.
 11. Kutoa taarifa za utekelezaji wa kazi.
 12. Kuratibu mambo yahusuyo maonyesho ya kitaifa na kimataifa
 1. Kusimamia kazi ya kujibu hoja za ukaguzi.
 2. Kusimamia uandaaji wa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha.
 3. Kusimamia maandalizi ya taarifa za ukaguzi wa fedha za mwaka.
 4. Kusimamia, kuthibitisha na kuidhinisha malipo.
 5. Kusimamia uandaaji wa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha.
 6. Kutoa taarifa za robo mwezi, robo, nusu na mwaka za mapato na matumizi ya Baraza.
 7. Kuandaa bajeti ya mapato na matumizi ya Baraza.
 8. Kusimamia uandaaji wa taarifa zote za uhasibu na kuhakikisha kwamba zimewasilishwa panapohusika.
 9. Kupitia na kuandaa kanuni za fedha.
 1. Kutafsiri sheria, kanuni, taratibu na miongozo mbalimbali ya kiutumishi na kutoa ushauri juu ya utekelezaji wake.
 2. Kubuni na kuandaa vigezo vya kutumika kutambua na kukadiria mahitaji ya mafunzo.
 3. Kusimamia uandaaji taarifa za mishahara ya watumishi.
 4. Kutekeleza sheria zinazohusu haki na maslahi ya wafanyakazi.
 5. Kusimamia uundaji wa Baraza la wafanyakazi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu.
 6. Kufuatilia, kuweka pamoja kumbukumbu, na kushughulikia maslahi ya watumishi wanaostaafu.
 7. Kuratibu utekelezaji wa mipango ya mafunzo.
 8. Kuandaa taarifa za kiutumishi na kuziwasilisha kwa mamlaka inayohusika.
 9. Kusimamia uhuishaji wa miundo ya utumishi.
 10. Kusimamia shughuli za utawala wa ofisi.
 11. Kusimamia tathmini ya utendaji kazi
 12. Kusimamia masuala ya nidhamu kazini.
 13. Kuandaa taarifa mbalimbali.