THEME:  Kiswahili - A pillar of Unity, Education and Economic Development.

How To


Those who wish to have their certificates translated should submit original copies and not photocopies of the certificates. For the languages for which the Council has experts, a certificate is translated for Tshs. 30,000/=. For the languages for which the Council lacks experts in translation, the council refers customers to approved external experts. External experts do the translation at the costs negotiated between the customer and the translator. The external translator shall sign his/her name on the translated documents and the customer shall submit the document to BAKITA for approval and stamping. The cost for approval is Tshs. 10,000/= for Tanzanians and 20 USD or Tshs. 40,000/= for non Tanzanians. For translation of manuscripts, books etc, the charge is Tshs. 30,000/= for a page of between 200 and 220 words. The customer is required to submit a hard copy and soft copy, if available. The Council shall issue a proforma invoice to the customer, and the customer shall be required to deposit 50% of the total costs as down payment before commencement of the work, and then clear the balance before he/she can take the translated document.
An individual, organization or institution which needs information on anything, including services offered by the Council can use the following modes:-
1. Visit the Council’s website, which is http://www.bakita.go.tz
2. Call 2762243
3. Write a letter to: The National Kiswahili Council P.O.Box 4766 Dar es- Salaam.
4. Write an e-mail to bakita@habari.go.tz
5. Visit BAKITA offices located in Kijitonyama, Block No. 45.B
The following are the procedures for issuing a customer with accreditation for his/her manuscript or book:
• Visit our office with the manuscript in a hard copy.
• The manuscript will be checked for the number of pages to determine charges, in which case Tshs. 5,000/= is charged for a page.
• After payments, the manuscript will be read through and then taken back to the customer to incorporate the recommended amendments.
• After incorporating the changes, the customer will take the book back to BAKITA for proof-reading to see that the reccommeded changes are duly incorporated.
• If the recommended changes are duly incorporated, the book or manuscript shall be stamped, and finally the customer is issued with a Certificate of Accreditation for his/her book, to certify that it is suitable for use by the targeted audience since the language used is formal and approved
An individual, organization, institution or company which finds it difficult accessing Kiswahili vocabulary relevant to their activities can send the English versions to BAKITA by phone, e-mail, or ordinary mail. However, an individual may visit BAKITA to obtain advice on anything about different Kiswahili vocabulary.
ow">
Kwa wale wanaotaka kutafsiriwa vyeti ni lazima watuletee nakala halisi na sio fotokopi. Kwa lugha ambazo Baraza lina wataalamu tunatafsiri kwa gharama ya Tsh 30,000 kwa cheti kimoja; Baraza linatumia wafasiri wa nje ambao wameidhinishwa kutafsiri lugha mbalimbali ambazo hatuna wataalamu wake ofisini. Mtaalamu wa nje anatafsiri kwa gharama atakazoelewana na mteja na kuandika jina na saini yake kwenye tafsiri na kisha mteja atatakiwa kuleta BAKITA kwa ajili ya kuthibitishiwa kwa kugongewa muhuri. Gharama za kugonga muhuri ni Tsh 10,000 kwa Mtanzania na Dola za Marekani 20 au Tsh 40,000 kwa mteja asiye Mtanzania. Kwa tafsiri ya miswada, vitabu n.k tunatoza Tsh 30,000 kwa ukurasa mmoja wenye maneno kuanzia 200 hadi 220. Mteja atatakiwa kuleta nakala mango (hard copy) na nakala tete (soft copy) kama anayo. Baraza litampatia Ankara Kifani (Proforma Invoice) ambapo atatakiwa kulipa asilimia 50 ya malipo yote kabla ya kazi kuanza, na kisha anapokuja kuchukua kazi atatakiwa kukamilisha asilimia 50 iliyobakia kabla ya kukabidhiwa kazi.
Mtu, shirika kampuni au taasisi inayohitaji kufahamishwa chochote au kujua namna ya kupata huduma zinazotolewa na Baraza inaweza kutumia njia zifuatazo:- 1. Tembelea tovuti ya Baraza ambayo ni http://www.bakita.go.tz 2. Kupiga simu Na. 2762243 3. Kuandika Barua kwa Anuani ifuatayo: Baraza la Kiswahili la Taifa S.L.P. 4766 Dar-Es- Salaam 4. Kuandika barua pepe ambayo ni bakita@habari.go.tz 5. Kufika katika ofisi za BAKITA zilizo Kijitonyama, kitalu Na. 45.B
Taratibu za kufuata wakati wa kumpatia mteja ithibati ya muswada au kitabu chake ni kama ifuatavyo: • Fika ofisini na muswada wako ukiwa katika nakala mango. • Muswada utakaguliwa idadi ya kurasa kwa ajili ya kulipia, ambapo gharama za malipo ni sh. 5000/= kwa kila ukurasa. • Baada ya kulipia, muswada utasomwa na hatimaye mteja atarudishiwa kitabu chake na kwenda kuingiza marekebisho aliyoshauriwa. • Ukisha kuingiza marekebisho hayo, atakirudisha tena kwa ajili ya kuhakikiwa kama umeingiza kwa usahihi marekebisho hayo, kadiri ya maelekezo uliyopewa. • Ikiwa marekebisho hayo yatakuwa yameingizwa kama ilivyoshauriwa, kitabu au muswada utagongwa muhuri na hatimaye mteja atapatiwa cheti cha ithibati kwa ajili ya kitabu chake, kuwa kinafaa kutumika kwa wadau aliokusudia kwa kuwa sasa kina lugha iliyo fasaha na iliyothibitishwa.
Mtu, shirika, taasisi au Kampuni ambayo inapata shida katika kupata istilahi za Kiswahili zinazoendana na shughuli zake iwasilishe istilahi hizo BAKITA kwa njia ya simu, barua pepe na kwa njia ya barua za kawaida. Aidha, mtu binafsi anaweza kuja BAKITA kupata ushauri wa chochote kinachohusiana na maneno mbalimbali ya Kiswahili.