KAULIMBIU:  Kiswahili - Mhimili wa Umoja, Maendeleo ya Elimu na Uchumi.

KUPATA HUDUMA YA TAFSIRI


Kwa wale wanaotaka kutafsiriwa vyeti ni lazima watuletee nakala halisi na sio fotokopi. Kwa lugha ambazo Baraza lina wataalamu tunatafsiri kwa gharama ya Tsh 30,000 kwa cheti kimoja; Baraza linatumia wafasiri wa nje ambao wameidhinishwa kutafsiri lugha mbalimbali ambazo hatuna wataalamu wake ofisini. Mtaalamu wa nje anatafsiri kwa gharama atakazoelewana na mteja na kuandika jina na saini yake kwenye tafsiri na kisha mteja atatakiwa kuleta BAKITA kwa ajili ya kuthibitishiwa kwa kugongewa muhuri. Gharama za kugonga muhuri ni Tsh 10,000 kwa Mtanzania na Dola za Marekani 20 au Tsh 40,000 kwa mteja asiye Mtanzania. Kwa tafsiri ya miswada, vitabu n.k tunatoza Tsh 30,000 kwa ukurasa mmoja wenye maneno kuanzia 200 hadi 220. Mteja atatakiwa kuleta nakala mango (hard copy) na nakala tete (soft copy) kama anayo. Baraza litampatia Ankara Kifani (Proforma Invoice) ambapo atatakiwa kulipa asilimia 50 ya malipo yote kabla ya kazi kuanza, na kisha anapokuja kuchukua kazi atatakiwa kukamilisha asilimia 50 iliyobakia kabla ya kukabidhiwa kazi.Nifanyeje?

KUPATA HUDUMA YA TAFSIRI

Kwa wale wanaotaka kutafsiriwa vyeti ni lazima watuletee nakala halisi na sio fo.......

HUDUMA ZINAZOHUSU BARAZA KWA UJUMLA

Mtu, shirika kampuni au taasisi inayohitaji kufahamishwa chochote au kujua.......

KUPATIWA ITHIBATI YA KITABU

Taratibu za kufuata wakati wa kumpatia mteja ithibati ya muswada au kit.......