KAULIMBIU:  Kiswahili - Mhimili wa Umoja, Maendeleo ya Elimu na Uchumi.

MAFUNZO YA KISWAHILI KWA WAGENI


Imechapishwa Jumatano, 24 Mei 2017Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) linapenda kuutangazia umma kuwa kuanzia mwezi Oktoba 2016, litaanza rasmi kutoa mafunzo ya Kiwango cha Awali ya Kiswahili kwa Wageni. Kozi ya Mafunzo haya itafanyika kwa muda wa wiki sita (6) kuanzia tarehe ambayo mwanafunzi atajisajili.
Utoaji wa mafunzo ya Kiswahili kwa Wageni ni moja ya majukumu ya BAKITA katika kueneza, kusimamia na kuratibu ukuaji na maendeleo ya Kiswahili duniani.
Wageni kutoka ndani na nje ya Afrika wanakaribishwa sana kwa ajili ya kujifunza Kiswahili.
Mafunzo haya yatatolewa na walimu wa lugha wabobezi na mwanafunzi ataweza kuzungumza Kiswahili kwa muda mfupi sana. Usikose nafasi hii muhimu!
Mafunzo haya yatafanyika kwenye ofisi zake zilizoko Makumbusho/Kijitonyama karibu na Kituo cha Daladala cha Makumbusho.
Usikiapo tangazo hili mjulishe na mwenzako.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Baraza kwa:
Simu: +255 22 2762213 au +255 22 2762243
Simu ya mkononi: +255 783 544 441 au +255 754 578197
Baruapepe: Bakita@habari.go.tz