Tanzania emblem

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Baraza la Kiswahili la Taifa
Tanzania emblem
Connect with us

Habari na Matukio

BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA) KUWA NA KANZIDATA YA WATAALAMU WA KISWAHILI

Published

on

Baraza la Kiswahili la Taifa lilifanya mkutano na waandishi wa habari tarehe 28/08/2017 kufafanua tangazo lake lilitolewa katika mitandao ya kijamii. Tangazo lake lilihusu uanzishaji wa kanzidata ya wataalamu wa Kiswahili.

Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) Dkt. Selemani S. Sewangi aliwaeleza waandishi wa habari azima ya Baraza ya kuwa na kanzidata ya wataalamu wa Kiswahili. Alieleza kwamba, kuwa na wataalamu wa Kiswahili ni jambo moja na kuwa na taarifa zao ambazo zinaweza kupatikana haraka pindi zitakapohitajika ni jambo jingine. Pamoja na kwamba Tanzania ina wasomi na wataalamu wengi wa Kiswahili, leo hii sio rahisi kujua wataalamu hao ni kinanani, wana ujuzi wa aina gani na wa kiwango gani, wako wapi na wanafanya nini. Katika hali kama hiyo, sio rahisi kuwapata wataalamu hao pale uhitaji wa haraka unapojitokeza.

Alieleza kwamba ili kukabiliana na tatizo hilo, BAKITA limeamua kukukusanya taarifa za kitaaluma na za kibinafsi za wataalamu wa Kiswahili na kuzihifadhi katika mfumo wa kikompyuta ambao utawezesha kupatikana kwa wataalamu hao pale watakapokuwa wakihitajika.

Taarifa zinazokusanywa ni vivuli vya vyeti vya matokeo ya kuhitimu katika vyuo vikuu na katika taasisi nyingine za mafunzo ya utaalamu husianifu kama vile utaalamu wa ukalimani, tafsiri, ualimu wa Kiswahili kwa wageni na ukalimani wa lugha ya alama kwa Kiswahili. Aidha, wasifu (CV) wa wataalamu hao wenye taarifa mbalimbali kama vile, namba zao za simu, anuani za barua pepe, hali yao ya ajira, lugha nyingine za kimataifa wanazozijua, uzoefu wao katika ajira mbalimbali zinazohusiana na Kiswahili utatakiwa.
Kwa sababu lengo ni kukusanya taarifa za kitaaluma na za kiutaalamu, katika zoezi hili vivuli vya vyeti vya matokeo ya Sekondari, vyeti vya uanachama wa vyama vya Kiswahili, vyeti vya kuhudhuria makongamano na hata vyeti vya kuhitimu havitahitajika.

Taarifa hizo zitairahisishia Serikali kuwapata wataalamu wetu wa Kiswahili na utaalamu husianifu pale itakapowahitaji, ama katika ajira au kwa majukumu mengine ya kitaifa. Vilevile utalirahisishia BAKITA katika uraribu wa mambo mbalimbali yanayohusu wataalamu hao ikiwa ni pamoja na kufanikisha mipango ya mafunzo ya muda mfupi ya msasa katika utaalamu mbalimbali.
Aidha, Dkt. Selemani Sewangi alifafanua kwamba mahitaji ya wataalamu wa Kiswahili kwa hivi sasa yameongezeka sana na hivyo ni muda mwafaka kuwa na kanzidata ya wataalamu hawa ili kuhakikisha kwamba mara tu wanapohitajika wanapatikana. Pia, alitoa mfano wa viongozi mbalimbali waliotembelea nchi yetu mfano Waziri Mkuu wa Ethiopia Heilemariam Dessalegn na Rasi wa Misri Abdel Fattah Elsisi ya kwamba wote walionyesha nia ya kupatiwa walimu wa kwenda kufundisha Kiswahili katika nchi zao.
Alisema kuwa taarifa zilizoainishwa hapo juu zinatakiwa kutumwa kwenye barua pepe ya BAKITA ambayo ni bakita@habari.go.tz na aliwahakikishia wataalamu hao kwamba taarifa zao zitapokelewa na kushughulikiwa inavyopaswa.

Kaimu Ofisa Mawasiliano na Umma,
BAKITA

Continue Reading

Habari na Matukio

MAFUNZO YA KISWAHILI KWA WAGENI

Published

on

BARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA) LINATOA MAFUNZO YA KUIMARISHA STADI ZA KUFUNDISHA KISWAHILI KWA WAGENI SAMBAMBA NA KUTAMBUA RASMI WALIMU WA KISWAHILI KWA WAGENI. MAFUNZO HAYA NI ENDELEVU, NA YANAFANYIKA DAR ES SALAAM NA KATIKA MIKOA KWA RATIBA IFUATAYO;
1. ARUSHA
KUANZIA: MEI 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA:
I. Ndugu. NELSON MHADHIRI WA CHUO KIKUU CHA ARUSHA
SIMU: 0752495167
2. MOROGORO
KUANZIA: APRILI 22 -26/ 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
I. ZAKIA ISMAIL KIMVULE
SIMU: 0712466673
3. MWANZA (AWAMU YA 2)
KUANZIA: MEI 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
I. ZAKARIA EMMANUEL
SIMU: 0755350165
4. MBEYA (AWAMU YA 2)
KUANZIA: JUNI 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
I.EDMUND MWANDEMELE
SIMU: 0756390305
5. IRINGA
KUANZIA: APRILI 15 – 19/ 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
I. LUCAS CHUNGA
SIMU: 0745108144
6. KILIMANJARO
KUANZIA: MEI 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
CHEDIEL MNJOKAVA
SIMU: 0786538223/0758754270
7. TANGA
KUANZIA: MEI 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
I. MWAJUMA SELEMAN MWL. WA SHULE YA SEKONDARI OLD TANGA
SIMU: 0713689868
8. LINDI
KUANZIA: JUNI 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
I. FURAHA WILLY
SIMU: 0789608252/ 0764546393
9. KAGERA
KUANZIA: JUNI 2019
KWA MAELEZO ZAIDI WASILIANA NA NDUGU:
I. EPMACHIUS K. AUDAX
SIMU: 0766828028
II. CHRISTOM H. MAPUNDA
SIMU: 0764711735

LENGO: KUWEZESHA SERIKALI KUTAMBUA IDADI YA WATAALAMU WA KISWAHILI ILIYONAO NA KUWEZESHA UPATIKANAJI WAO PALE WANAPOHITAJIKA NDANI NA NJE YA NCHI. WASHIRIKI WOTE WA MAFUNZO HAYA WATAINGIZWA KWENYE KANZIDATA YA WATAALAMU WA KISWAHILI..
WAHUSIKA: WATAALAMU WA KISWAHILI WENYE ELIMU YA KUANZIA SHAHADA YA KWANZA HADI YA UZAMIVU.
ADA: SHILINGI LAKI MOJA NA ELFU ISHIRINI TU (120,000) KWA MIKOANI
MUDA WA MAFUNZO: WIKI MOJA
MALIPO: WASILIANA NA OFISI YETU YA UHASIBU BAKITA: 0757979611 ILI KUPATA BILI YA MALIPO.
“KISWAHILI UHAI WETU UTASHI WETU”
KARIBUNI SANA
Usikiapo tangazo hili mjulishe na mwenzako.
Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Baraza kwa:
Simu: +255 22 2762213 au +255 22 2762243
Simu ya mkononi: +255 783 544 441 au +255 754 578197
Baruapepe: Bakita@habari.go.tz

Continue Reading

Habari na Matukio

MAFUNZO YA KUTAMBUA VIPAJI VYA UKALIMANI

Published

on

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) kwa kushirikiana na wakalimani wabobezi litatoa mafunzo ya siku tatu ya kutambua vipaji vya ukalimani. Mafunzo yatatolewa katika mazingira yenye vifaa vyote muhimu vya ukalimani. Kila mshiriki atafanya ukalimani kwa vitendo na kufanyiwa tathminiya uwezo wake wa kukalimani.

Wakalimani watakaobainika kuwa na uwezo mzuri watatambuliwa rasmi na BAKITA na kuandaliwa mipango kabambe ya kuimarisha uwezo wao, ikiwa ni pamoja na kuanza kutumika katika kutoa huduma hiyo ya ukalimani.

Sifa za Mshiriki:

Kijana wa Kitanzania mwenye uwezo wa kuwa mkalimani katika lugha zifuatazo:

  1. Kiswahili –Kiingereza – Kiswahili
  2. Kiswahili –Kifaransa – Kiswahili
  3. Kiswahili – Kireno –Kiswahili
  4. Kiswahili – Kiarabu –Kiswahili

Gharama ya Kushiriki

Kila mshiriki atalipa shilingi laki moja na elfu thelethini tu (130,000/=) kwa ajili ya kuchangia gharama za kukodisha vifaa vya ukalimani, ukumbi na chakula kwa siku tatu za mafunzo.Malipo yatafanyika kupitia Benki ya NMB au kwa SIMU baada ya mlipaji kupewa namba ya kumbukumbu ya malipo.

Mahali, Tarehe na Muda wa mafunzo

Mafunzo yatatolewa katika Ofisi za BAKITA Kijitonyama, Tarehe 21– 23/10/2019 kuanzia saa 4.00 asubuhi hadi 10.00 jioni.

Idadi ya washiriki:

Kutokana na vifaa tulivyonavyo, tutaanza na washiriki 25 tu. Kwa wale walio tayari kushiriki katika awamu hii ya kwanza tafadhali wasiliana na Mratibu wa Mafunzo, Bw. Arnold Msofe (0762 020227).

Trending