Haya ni mafunzo ya utangulizi ambayo yana lengo la kuitambulisha lugha ya Kiswahili na Utamaduni wake kwa washiriki. Kozi hii itamwezesha mjifunzaji kufanya mawasiliano ya msingi na ya kawaida katika Kiswahili
Maeneo muhimu ni kama salamu, kujitambuslisha, na maelezo rahisi ya maisha ya kila siku. Kupitia mbinu mbalimbali za ufundishaji kama vile maigizo dhima, utendaji na michezo ya lugha shirikishi, mjifunzaji atajifunza msamiati wa msingi unaohusiana na hali na matukio ya kila siku na kuchunguza mada zinazolenga kukutambulisha kwa kanuni za kijamii na kiutamaduni za Kitanzania.
Pamoja na shughuli za darasani, mjifunzaji atashiriki katika ziara za kimasomo na shughuli mbalimbali za kijamii ambazo zinalenga kumzamisha kindakindaki katika jamii ili aweze kuzungumza Kiswahili katika mazingira halisi.
Salamu, kujitambulisha, kuwatambulisha wanafamilia, kuagiza vyakula na vinywaji, kukubaliana bei na kununua dukani au sokoni, kuongelea mambo ya sasa, yaliyopita na yajayo, kusoma saa kwa Kiswahili, kuzungumzia kazi au utaalamu, kuzungumzia matatizo ya kiafya, kutoa na kupokea maelekezo, kuelekeza mahali alipo au kilipo kitu fulani.
Ni watu wasio na ujuzi wa lugha ya Kiswahili, ambao wanaweza kuwa: