Tanzania emblem

Jamuhuri ya Mungano wa Tanzania


Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)

Tanzania emblem

Sehemu za BAKITA

Majukumu ya sehemu hii ni:
 1. Kutoa huduma za tafsiri na ukalimani ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 2. Kuratibu na kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa ajili ya kujenga na kuimarisha uwezo wa wafasiri na wakalimani wa ndani
 3. Kuandika makala na maandiko mengine kuhusiana na tafsiri na ukalimani
 4. Kuandaa kanzidata ya wafasiri na wakalimani ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
 5. Kudhibiti ubora wa kazi za tafsiri na ukalimani
 6. Kupitia na kuthibitisha tafsiri zilizofanywa na taasisi mbalimbali au mawakala wa BAKITA
 7. Kufanya tafiti za masuala ya tafsiri na ukalimani

Majukumu ya sehemu hii ni:

 1. Kuandaa msamiati na istilahi zinazotakiwa kusanifiwa, kuratibu usanifishaji wake na kuzisambaza
 2. Kuandika kamusi za jumla na mahususi kwa ajili ya matumizi ya taaluma mbalimbali
 3. Kufanya utafiti kuhusiana na kamusi na istilahi mbalimbali
 4. Kuandika makala na maandiko mengine kuhusiana na kamusi na istilahi; Kutoa mafunzo ya muda mfupi ya uandaaji wa kamusi na istilahi kwa wanaohitaji
 5. Kukusanya maneno kutoka kwenye maandiko ya Kiswahili na kuyaingiza kwenye Kongoo ya Kiswahili ya Taifa.

Majukumu ya sehemu hii ni

 1. Kuratibu utayarishaji na utekelezaji wa Mpango Mkakati wa Maendeleo ya Muda wa Kati, Mipango Kazi na Bajeti ya Mwaka kulingana na bajeti ya Serikali
 2. Kufanya ufuatiliaji na tathmini ya mipango ya Baraza
 3. Kuandaa ripoti za utekelezaji wa miradi, programu na ,mipango kazi
 4. Kusimamia uandaaji na utekelezaji wa programu za uwekezaji za Baraza
 5. Kufanya tafiti za shughuli mbalimbali za Baraza
 6. Kuandaa na kutekeleza mikakati ya uhamasishaji wa matumizi ya rasilimali

Majukumu ya sehemu hii ni:

 1. Kupitia na kutoa ithibati ya matumizi sahihi ya Kiswahili katika maandiko mbalimbali
 2. Kutoa mafunzo ya Kiswahili kwa wageni
 3. Kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa watu wenye mahitaji maalumu kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili
 4. Kutoa mafunzo ya muda mfupi ya mbinu za uhariri kwa wanaohitaji
 5. Kuandika makala na maandiko mengine kuhusu lugha na fasihi ya Kiswahili
 6. Kufanya tafiti na kutoa machapisho kuhusu fasihi ya Kiswahili
 7. Kuhariri vitabu, miswada na maandiko mengine ya Kiswahili
 8. Kuandaa mashindano ya uandishi wa lugha ya Kiswahili katika ngazi mbalimbali za elimu
 9. Kuendesha na kuratibu mafunzo kwa wanafunzi wanaofanya kazimradi zinazohusiana na lugha ya Kiswahili
 10. Kuratibu na kuendeshaa maonesho ya utamaduni.

Majukumu ya Sehemu ya Uhasibu ni:

 1. Kukusanya na kusimamia mapato
 2. Kufanya upatanisho wa Kibenki
 3. Kuandaa Hesabu za Mwaka na Taarifa zingine za Kifedha
 4. Kushughulikia miamala ya fedha taslimu na hundi
 5. Kuweka kumbukumbu/kufanya upatanisho wa masurufu yote yanayotolewa
 6. Kujibu hoja za ukaguzi
 7. Kutoa taarifa ya mapato na matumizi ya Baraza kwa mwezi, robo, nusu na mwaka
 8. Kusimamia maandalizi ya kumbukumbu zote za hesabu na kuhakikisha kuwa zimewasilishwa mahali husika
 9. Kuandaa na kupitia kanuni za kifedha