Tanzania emblem

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania


Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)

Tanzania emblem
Dondoo
Dira na Dhima 1.0 Dira Kuwa taasisi yenye nguvu kisheria, kifedha na kutambulika kitaifa na kimataifa katika kuratibu na kusimamia maendeleo ya lugha ya Kiswahili. 2.0 Dhima Kukuza, kuendeleza na kuhimiza matumizi fasaha na sanifu ya Kiswahili ndani na nje ya nchi kwa kushirikiana na wadau wengine.

Kuhusu BAKITA

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA) ni Shirika la Umma ambalo kwa kawaida huwa chini ya Wizara yenye dhamana ya Utamaduni. Baraza liliundwa kwa Sheria ya Bunge Na. 27 ya mwaka 1967 pamoja na marekebisho yake ya mwaka 1983 na 2016. Sheria hii inalipa Baraza mamlaka ya kusimamia na kuratibu shughuli za wadau wote wanaokuza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Baraza liliundwa kutokana na mapendekezo makuu ya Kamati iliyoundwa kwenye kikao cha wataalamu wa lugha kilichoitishwa na Waziri wa Elimu Disemba 1961. Lengo la kikao hicho lilikuwa ni kutoa mapendekezo yatakayosaidia kuinua Kiswahili kama lugha ya Taifa. Baraza lilianza kazi na watumishi wanne katika ofisi za Wizara ya Elimu. Miongoni mwa kazi ya kwanza ya Baraza ilipendekezwa iwe kufasiri msamiati na misemo ya Sheria. Baadaye mwaka 1972, Baraza lilipata ofisi zake katika jengo la Shirika la Nyumba la Taifa, mtaa wa Samora na Azikiwe jijini Dar es Salaam, na mwaka 2012 Baraza lilihamia Kitalu Na.45 B, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Huduma Zitolewazo na BAKITA

Huduma ya Ushauri kwa wanafunzi na watafiti

Soma Zaidi>>

Huduma ya Kutoa ithibati ya lugha

Soma Zaidi>>

Huduma za Tafsiri na Ukalimani

Soma Zaidi>>

Usambazaji wa Istilahi za Kiswahili

Soma Zaidi>>

Habari Mpya

  • 8th Feb 2023

MAFUNZO YA KISWAHILI KWA WAGENI

Soma zaidi
  • 8th Feb 2023

MATUKIOBARAZA LA KISWAHILI LA TAIFA (BAKITA) KUWA NA KANZIDATA YA WATAALAMU WA KISWAHILI

Soma zaidi
  • 8th Feb 2023

MAFUNZO YA KUTAMBUA VIPAJI VYA UKALIMANI

Soma zaidi

Matangazo

Machapisho

18th Sep 2023 | articles
test
15th Mar 2023 | publications
MKATABA WA HUDUMA KWA MTEJA

Vitabu vya BAKITA

Maneno ya Mtandaoni

Neno: Afiriti

Maana: Mtu anayechochea wenzake kufanya uovu

Mfano:Afiriti amewasababishia wenzake kifungo

Neno: Belenga

Maana: Tembea kwa maringo na kujidai kwingi

Mfano:Mfano: Warembo wanabelenga jukwaani.

Neno: Wekua

Maana: Toa fedha kwenye akaunti ya benki

Mfano:Mfano: Ninakwenda kuwekua fedha kwa ajili ya matumizi ya nyumbani.