MHANDISI HERSI ATEULIWA BALOZI WA KISWAHILI TANZANIA

10 Apr, 2026
MHANDISI HERSI ATEULIWA BALOZI WA KISWAHILI TANZANIA

Mhandisi Hersi Said, raisi wa klabu ya Yanga na mjumbe wa Kamati ya mashindano ya wanaume upande wa vilabu Afrika katika Shirikisho la mpira wa miguu (CAF)ameteuliwa kuwa balozi wa Kiswahili Tanzania, akibeba dhamira ya kuunganisha hadhi ya lugha ya Kiswahili na sekta ya michezo. 

 “Jukumu la kukienzi na kukitunza Kiswahili ni letu sote,” Asema Mhandisi Hersi.

Kupitia nafasi yake CAF kama mjumbe wa Kamati ya Mashindano ya Vilabu upande wa wanaume Afrika, anakusudia kukitangaza Kiswahili ndani na nje ya mipaka ya Tanzania na kukipa hadhi inayostahili Kimataifa.

Balozi Mhandisi Hersi ataendelea kushirikiana na Baraza la Kiswahili la Taifa katika kuhakikisha lugha ya Kiswahili inatambulika na kuheshimika duniani kote. Hatua hii inaendana na jukumu la msingi la BAKITA la kukuza, kuendeleza na kusimamia matumizi bora ya Kiswahili.