Category Title
Maadili ya Msingi
Ili Baraza liwe katika mazingira yanayoliwezesha kufikia malengo yake ya kukuza na kusimamia maendeleo ya Kiswahili ndani na nje ya nchi, yafuatayo yatakuwa maadili ya msingi: -
(i) Kukuza ushiriki wa jamii: Kukuza ushiriki wa jamii kuhusu matumizi ya Kiswahili fasaha katika matumizi rasmi;
(ii) Utendaji wa pamoja: Kufanya kazi kwa pamoja kama timu ili kufikia malengo ya Baraza na jamii kwa ujumla;
(iii) Kufanya kazi kwa bidii: Kuongeza juhudi katika kutoa huduma na kuzingatia ubora wa huduma zinazotolewa;
(iv) Uadilifu: Kuwa waadilifu na mfano wa kuigwa katika utendaji kazi;
(v) Uwajibikaji: Kufanya kazi kwa juhudi na maarifa ili kukuza na kueneza lugha ya Kiswahili ndani na nje ya nchi;
(vi) Matumizi bora ya rasilimali: Kutumia kwa uangalifu rasilimali za Baraza kwa manufaa na maendeleo ya lugha ya Kiswahili;
(vii) Uwazi: Kuzingatia uwazi wakati wa utekelezaji wa majukumu ya Baraza na kuwa tayari kupokea maoni ya jamii; na
(viii) Kukubaliana na mabadiliko: Kuwa tayari wakati wote ili kuendana na mabadiliko.
